ملة الإسلام

السورة 81 · 29 آية · Ali Muhsin Al Barwani

سورة التكوير باللغة السواحلية

السورة بالعربية مع التفسير استمع إلى سورة التكوير (1,316 قارئاً)
مكيةسورة التكوير٢٩ آية

بِسۡمِ ٱللَّهِ ٱلرَّحۡمَٰنِ ٱلرَّحِيمِ

إِذَا ٱلشَّمۡسُ كُوِّرَتۡ ١Jua litakapo kunjwa وَإِذَا ٱلنُّجُومُ ٱنكَدَرَتۡ ٢Na nyota zikazimwa وَإِذَا ٱلۡجِبَالُ سُيِّرَتۡ ٣Na milima ikaondolewa وَإِذَا ٱلۡعِشَارُ عُطِّلَتۡ ٤Na ngamia wenye mimba pevu watakapo achwa wasishughulikiwe وَإِذَا ٱلۡوُحُوشُ حُشِرَتۡ ٥Na wanyama wa mwituni wakakusanywa وَإِذَا ٱلۡبِحَارُ سُجِّرَتۡ ٦Na bahari zikawaka moto وَإِذَا ٱلنُّفُوسُ زُوِّجَتۡ ٧Na nafsi zikaunganishwa وَإِذَا ٱلۡمَوۡءُۥدَةُ سُئِلَتۡ ٨Na msichana aliye zikwa hai atapo ulizwa بِأَيِّ ذَنۢبٍ قُتِلَتۡ ٩Kwa kosa gani aliuliwa وَإِذَا ٱلصُّحُفُ نُشِرَتۡ ١٠Na madaftari yatakapo enezwa وَإِذَا ٱلسَّمَآءُ كُشِطَتۡ ١١Na mbingu itapo tanduliwa وَإِذَا ٱلۡجَحِيمُ سُعِّرَتۡ ١٢Na Jahannamu itapo chochewa وَإِذَا ٱلۡجَنَّةُ أُزۡلِفَتۡ ١٣Na Pepo ikasogezwa عَلِمَتۡ نَفۡسٌ مَّآ أَحۡضَرَتۡ ١٤Kila nafsi itajua ilicho kihudhurisha فَلَآ أُقۡسِمُ بِٱلۡخُنَّسِ ١٥Naapa kwa nyota zinapo rejea nyuma ٱلۡجَوَارِ ٱلۡكُنَّسِ ١٦Zinazo kwenda, kisha zikajificha وَٱلَّيۡلِ إِذَا عَسۡعَسَ ١٧Na kwa usiku unapo pungua وَٱلصُّبۡحِ إِذَا تَنَفَّسَ ١٨Na kwa asubuhi inapo pambazuka إِنَّهُۥ لَقَوۡلُ رَسُولٍ كَرِيمٍ ١٩Kwamba hakika bila ya shaka hii ni kauli ya Mjumbe mtukufu ذِي قُوَّةٍ عِندَ ذِي ٱلۡعَرۡشِ مَكِينٍ ٢٠Mwenye nguvu na mwenye cheo kwa huyo Mwenye Kiti cha Enzi مُّطَاعٍ ثَمَّ أَمِينٍ ٢١Anaye t'iiwa, tena muaminifu وَمَا صَاحِبُكُم بِمَجۡنُونٍ ٢٢Na wala huyu mwenzenu hana wazimu وَلَقَدۡ رَءَاهُ بِٱلۡأُفُقِ ٱلۡمُبِينِ ٢٣Na hakika yeye alimwona kwenye upeo wa macho ulio safi وَمَا هُوَ عَلَى ٱلۡغَيۡبِ بِضَنِينٍ ٢٤Wala yeye si bakhili kwa mambo ya ghaibu وَمَا هُوَ بِقَوۡلِ شَيۡطَٰنٍ رَّجِيمٍ ٢٥Wala hii si kauli ya Shetani maluuni فَأَيۡنَ تَذۡهَبُونَ ٢٦Basi mnakwenda wapi إِنۡ هُوَ إِلَّا ذِكۡرٌ لِّلۡعَٰلَمِينَ ٢٧Haikuwa hii ila ni ukumbusho kwa walimwengu wote لِمَن شَآءَ مِنكُمۡ أَن يَسۡتَقِيمَ ٢٨Kwa yule miongoni mwenu anaye taka kwenda sawa وَمَا تَشَآءُونَ إِلَّآ أَن يَشَآءَ ٱللَّهُ رَبُّ ٱلۡعَٰلَمِينَ ٢٩Wala nyinyi hamtataka isipo kuwa atake Mwenyezi Mungu Mola Mlezi wa walimwengu wote

الترجمة: Ali Muhsin Al Barwani.