ملة الإسلام

السورة 111 · 5 آية · Abdullah Muhammad Abu Bakr

سورة المسد باللغة السواحلية

السورة بالعربية مع التفسير استمع إلى سورة المسد (1,267 قارئاً)
مكيةسورة المسد٥ آية

بِسۡمِ ٱللَّهِ ٱلرَّحۡمَٰنِ ٱلرَّحِيمِ

تَبَّتۡ يَدَآ أَبِي لَهَبٍ وَتَبَّ ١Imehasirika mikono miwili ya Abu Lahab, na yeye mwenyewe ameangamia, kwa kumuudhi Mtume, rehema ya Mwenyezi Mungu na amani zimshukie. Hasara ya Abu Lahab ilithubutu مَآ أَغۡنَىٰ عَنۡهُ مَالُهُۥ وَمَا كَسَبَ ٢Hayakumfalia kitu mali yake na watoto wake. Kwani hivyo havitamkinga na adhabu ya Mwenyezi Mungu pindi ikimshukia سَيَصۡلَىٰ نَارًا ذَاتَ لَهَبٍ ٣Ataingia kwenye Moto wenye kuroroma وَٱمۡرَأَتُهُۥ حَمَّالَةَ ٱلۡحَطَبِ ٤yeye na mke wake ambaye alikuwa akibeba miba na kuiweka kwenye njia anayopita Mtume, rehema ya Mwenyezi Mungu na amani zimshukie, ili kumuudhi فِي جِيدِهَا حَبۡلٌ مِّن مَّسَدِۭ ٥Kwenye shingo yake patakuwa na kamba imara ya lifu gumu lilio kavu; atabebewa nayo kwenye Moto wa Jahanamu, kisha atarushwa nayo mpaka chini

الترجمة: Abdullah Muhammad Abu Bakr.